ABOUT US

ABOUT US.

Historia ya uwanzishwaji wa wilaya ya Lushoto sambamba na Halmashauri ya Lushoto
Kuthubutu katika katika kujiletea maendelea kulianza mara baada ya kuvunjwa kwa eneo la kiutawala lilloachwa na wakoloni kabla ya uhuru ambalo lilijulikana  kama " province",eneo hili lilijumuisha wilaya ya  Korogwe,Handeni,Kilindi , Same,na Mwanga.Mabadiliko hayo yalifanyikaikiwa ni hatua muhimu ya Utekelezaji wa mafaniko ya awali kabisa ya matakwa ya sheria za serikali za mitaa ya mwaka 1962 kifungu cha 333 iliyopitishwa na Bunge  la Tanganyika wakati huo.Mabadiliko hayo  yalizaa wilaya  mpys ya Lushoto ilikwenda sambamba  na uanzishwaji wa Halmashuri ya Lushoto  rasmi tarehe 29 Juni 1962 kabla haijagawanyika tena na kuzaa Halmashauri mbili  Lushoto na Bumbuli Mwaka 2013.
Eneo la Utawala
Halmashauri ya Lushoto  ipo kaskazini  mwa  Mkoa wa Tanga kati ya Latitude 4 25'-4 55' kusini mwa Ikweta na Longitude 30 10'-38 35' Mashariki mwa Longitudo kuu.Kijiografia wilaya Wilaya imepakana na nchi ya Kenya kwa upande wa kaskazini Mashariki,Wilaya ya Same (Mkoa wa Kilimanjaro Kwa upande wa kaskazini Magharibi,Wilaya ya Korogwe kwa upande wa kusini ,Halmashauri ya Bumbuli upande wa kusini Mashariki ,Kwa upande wa Mashariki ya mbali imepakana na Muheza na Mkinga
Halmashauri ya Lushoto inaeneo la ukubwa  wa kilometre za  mraba 2,300 km2 ( Hekta 227,371.43) sawa na asilimia 8.41 ya eneo lote la mkoa  wa Tanga
Utawala
Halmashauru ina Tarafa 5 Kata 33 vijii 125 pamoja na Vitongoji 948. Makau makuu ya Halmashuri ya Lushoto yako  Mjini Lushoto. Halmashauri imegawanyika katika majmbo mawili ya Uchaguzi Lushoto  na Mlalo.
Dira
Nikuwa na Jamii yenye uwezo wa kufikia huduma endelevu za jamii na kiuchumi 
Dhima
Kutoa huduma bora za kijamii na kiuchumi kwa kutumia rasilimali zilizopo kupitia Utawala bora
IDADI NA MTAWANYIKO WA WATU KATIKA MAENEO MBALI MBALI YA HALMASHAURI YA LUSHOTO
Demografia ya Halmashauri ya Lushoto ilikuwa ikiongezeka kwa ukubwa tangu 2002 kutoka 279,096 mpaka 332,436 mwaka 2012, Katika sensa ya  2002 Halmashauri ilikuwa ina idadi ya watu 279,096(125,353 wakiwa wanaume) na (153,743 wakiwa wanawake) katika sensa ya  mwaka 2012 ukiondoa Halmashauri ya Bumbuli Halmashauri ya Lushoto ina idadi ya watu 332,436 (153,847 wakiwa wanaume na 178,589 wakiwa wanawake